Posts

Putin anatuma ujumbe kwa Magharibi na taarifa za mafundisho ya nyuklia - Kremlin

 Putin anatuma ujumbe kwa Magharibi na taarifa za mafundisho ya nyuklia - Kremlin "Huu ni ujumbe unaozionya nchi hizi juu ya madhara yatakayoshiriki katika kuishambulia nchi yetu kwa njia mbalimbali, si lazima nyuklia," Dmitry Peskov alisema. MOSCOW, Septemba 26. /../. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema matamshi kuhusu mafundisho ya nyuklia ya Urusi ambayo Rais wa Urusi Vladimir Putin alitoa siku ya Jumatano yanatuma ishara kwa nchi za Magharibi. "Huu unapaswa kutazamwa kama ujumbe fulani," Peskov aliwaambia waandishi wa habari, alipoulizwa ikiwa marekebisho ya fundisho la nyuklia la Urusi Putin alitangaza Jumatano inaweza kuwa ujumbe kwa Magharibi. "Huu ni ujumbe unaozionya nchi hizi juu ya madhara yatakayoshiriki katika kuishambulia nchi yetu kwa njia mbalimbali, si lazima nyuklia," Peskov aliendelea kusema.

Israel yazuia mikusanyiko kaskazini mwa nchi huku ikiendelea kushambulia Hezbollah

Image
  Israel yazuia mikusanyiko kaskazini mwa nchi huku ikiendelea kushambulia Hezbollah Chanzo cha picha, Reuters Israel imeanzisha mashambulizi ya anga nchini Lebanon na inazuia mikusanyiko katika mji wa Haifa na maeneo mengine ya kaskazini huku ikiendelea kushambulia maeneo yanayohusishwa na Hezbollah. Makumi ya ndege za kivita zilianza "kwa kiasi kikubwa" kushambulia kusini mwa Lebanon "kufuatia kugundulika kwa Hezbollah ikijiandaa kufyatua risasi kuelekea eneo la Israeli", msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Daniel Hagari alisema. Mashambulizi ya hivi punde zaidi ya Israel yanakuja siku moja baada ya kufanya shambulio la anga huko Beirut, ambalo IDF ilisema liliua dazeni ya makamanda wakuu wa Hezbollah. Lebanon ilisema watu 37 - wakiwemo watoto watatu - waliuawa . Serikali ya Marekani inawataka raia wake huko kuondoka "kupitia chaguzi za usafiri wa kibiashara wakati bado zinapatikana". Siku ya Ijumaa, makabiliano ya mapigano mpakani ...

Israel yaamuru kufungwa kwa siku 45 kwa ofisi ya Al Jazeera Ukingo wa Magharibi

Image
  Israel yaamuru kufungwa kwa siku 45 kwa ofisi ya Al Jazeera Ukingo wa Magharibi Chanzo cha picha, AlJAZEERA Vikosi vya Israel vimevamia ofisi za shirika la utangazaji la Al Jazeera huko Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kuamuru kufungwa kwa muda wa siku 45. Wanajeshi wa Israel wenye silaha na waliojifunika nyuso zao waliingia ndani ya jengo hilo mapema Jumapili wakati wa matangazo ya moja kwa moja. Watazamaji walitazama wanajeshi wakitoa agizo la kufungwa kwa mkuu wa ofisi hiyo katika Ukingo wa Magharibi Walid al-Omari ambaye aliisoma moja kwa moja ujumbe huo hewani. Israel ilivamia ofisi za Al Jazeera huko Nazareth na Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu mwezi Mei baada ya kulielezea shirika hilo la utangazaji lenye makao yake Qatar kuwa tishio kwa usalama wa taifa. "Kulenga waandishi wa habari kwa njia hii kila mara kunalenga kufuta ukweli na kuzuia watu kusikia ukweli," Omari alisema katika maoni yaliyoripotiwa na mwajir...

Trump akataa mjadala wa pili wa TV akisema 'umechelewa sana'

Image
  Trump akataa mjadala wa pili wa TV akisema 'umechelewa sana' Chanzo cha picha, Getty Images Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema hatashiriki katika mjadala wa pili wa televisheni kabla ya uchaguzi wa urais mwezi Novemba. Wakati Makamu wa Rais Kamala Harris, mgombea wa Chama cha Democratic , alikubali mwaliko wa mdahalo wa CNN tarehe 23 Oktoba, mgombea mteule wa Republican Trump aliambia mkutano kuwa "umechelewa" kwani upigaji kura tayari umeanza. Timu ya kampeni ya Harris ilisema kwamba kutokana na rais huyo wa zamani kudai kuwa alishinda mjadala wao wa awali huko Philadelphia mapema mwezi huu anapaswa kukubali. Kura za maoni zilizopigwa baada ya mkutano huo zilipendekeza kuwa wengi wa watazamaji waliamini kuwa makamu wa rais alimshinda mpinzani wake. Baada ya mjadala wa Septemba 10, Trump alisema hakutakuwa na mijadala zaidi. Akizungumza katika mkutano wa hadhara huko Wilmington, North Carolina siku ya Jumamosi, alidai ushindi katika mdahalo...

Israel na Hezbollah zashambuliana kwenye mpaka wa Lebanon

Image
  srael na Hezbollah zashambuliana kwenye mpaka wa Lebanon Chanzo cha picha, Reuters Iwapo ndio unajiunga na matangazo ya moja kwa moja ya leo, haya ndio tunayojua kufikia sasa kuhusu mapigano ya usiku kucha Msururu wa maroketi yalirushwa kaskazini mwa Israel kutoka Lebanon usiku kucha, na kutua ndani zaidi ya Israeli kuliko mashambulizi ya awali. Hezbollah inasema ililenga maeneo ya viwanda na kijeshi, na makumi ya nyumba ziliripotiwa kuharibiwa IDF inasema roketi nyingi zilinaswa na mifumo ya ulinzi wa anga Picha zilionekana kuonyesha moto katika eneo la makazi karibu na Haifa kaskazini mwa Israel baada ya kupigwa na roketi. Hakujawa na ripoti zozote za vifo Mapema Jumapili, Israeli ilifunga shule na kuzuia mikusanyiko ya watu katika maeneo mengi ya kaskazini mwa nchi na Milima ya Golan inayokaliwa na Israeli. Wakati huo huo, Israel ilisema ilifikia malengo ya Hezbollah siku ya Jumamosi, ikiwa ni pamoja na mael...

Waziri Mkuu wa Lebanon atoa wito kwa nchi kuchukua msimamo wa wazi juu ya 'mauaji ya kutisha'

Image
  Waziri Mkuu wa Lebanon atoa wito kwa nchi kuchukua msimamo wa wazi juu ya 'mauaji ya kutisha' Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock Waziri Mkuu wa Lebanon ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kuchukua msimamo wa wazi" juu ya kile anachoita "mauaji haya ya kutisha" katika taarifa iliyochapishwa leo . Waziri Mkuu Najib Mikati anasema alikuwa na nia ya kusafiri kwenda New York kushiriki katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lakini aliamua kutosafiri baada ya matukio ya wiki hii. "Ninasisitiza kwamba hakuna kipaumbele kwa sasa ambacho ni cha juu zaidi kuliko kukomesha mauaji yanayofanywa na adui - Israel na aina mbalimbali za vita wanavyoendesha," ilisema taarifa hiyo. "Pia natoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na ulimwengu kuchukua msimamowa wazi kuhusu mauaji haya ya kutisha." Mikati pia anatoa wito wa "kupitishwa kwa sheria za kimataifa ili kupunguza njia za kiteknolojia za kiraia kutoka kwa malengo ya kijeshi na ...

Takriban watu 51 wamefariki katika mlipuko wa mgodi wa makaa ya mawe nchini Iran

Image
  Takriban watu 51 wamefariki katika mlipuko wa mgodi wa makaa ya mawe nchini Iran Chanzo cha picha, APTN Mlipuko uliosababishwa na uvujaji wa gesi kwenye mgodi wa makaa ya mawe mashariki mwa Iran umeua takriban watu 51, vyombo vya habari vya serikali vilisema Jumapili. Zaidi ya wengine 20 walijeruhiwa baada ya mlipuko huo katika jimbo la Khorasan Kusini. Inaripotiwa kusababishwa na mlipuko wa gesi ya methane katika vitalu viwili vya mgodi huko Tabas, kilomita 540 (maili 335) kusini mashariki mwa mji mkuu Tehran. Mlipuko huo ulitokea saa 21:00 kwa saa za ndani (17:30 GMT) siku ya Jumamosi, vyombo vya habari vya serikali vilisema. Gavana wa Khorasan Kusini Javad Ghenaatzadeh alisema kulikuwa na wafanyikazi 69 kwenye vitalu wakati wa mlipuko huo. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, alisema: "Kulikuwa na mlipuko na kwa bahati mbaya watu 69 walikuwa wakifanya kazi katika vitalu vya B na C vya mgodi wa Madanjoo. "Katika kitalu C kulikuwa na watu 22 na katika kitalu B ...