Zaidi ya watu 70,000 waliojitolea kuipigania Urusi wafa Ukraine

 

Zaidi ya watu 70,000 waliojitolea kuipigania Urusi wafa Ukraine

Baadhi ya familia hazitoi hadharani maelezo ya vifo vya jamaa zao

Chanzo cha picha, Getty Images

Zaidi ya watu 70,000 wanaopigana katika jeshi la Urusi sasa wamefariki nchini Ukraine, kulingana na data iliyochambuliwa na BBC.

Na kwa mara ya kwanza, watu wa kujitolea raia ambao walijiunga na vikosi vya jeshi baada ya kuanza kwa vita, sasa wanaunda idadi kubwa zaidi ya watu waliouawa kwenye uwanja wa vita tangu uvamizi kamili wa Urusi uanze mnamo 2022.

Kila siku, majina ya waliouawa nchini Ukraine, kumbukumbu zao na picha kutoka kwa mazishi yao huchapishwa kote Urusi kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.

BBC Kirusi na tovuti huru ya Mediazona wamekusanya majina haya, pamoja na majina kutoka vyanzo vingine vya wazi, ikiwa ni pamoja na ripoti rasmi.

Tulikagua kufahamu taarifa hiyo ilikuwa imetolewa na mamlaka au jamaa za marehemu na kwamba walikuwa wametambuliwa kuwa walikufa katika vita.

Makaburi mapya pia yamesaidia kutoa majina ya wanajeshi waliouawa nchini Ukraine, haya huwa yana alama za bendera na shada za maua zinazotumwa na wizara ya ulinzi.

Tumetambua majina ya wanajeshi 70,112 wa Urusi waliouawa nchini Ukraine, lakini idadi halisi inaaminika kuwa kubwa zaidi.

Baadhi ya familia hazitoi hadharani maelezo ya vifo vya jamaa zao na uchanganuzi wetu haujumuishi majina ambayo hatukuweza kukagua, au vifo vya wanamgambo katika Donetsk inayokaliwa na Urusi na Luhansk mashariki mwa Ukraine.

Comments

Popular posts from this blog

Israel yazuia mikusanyiko kaskazini mwa nchi huku ikiendelea kushambulia Hezbollah

Mashambulizi ya Israel huko Lebanon yana athari gani?

Korea Kaskazini kupanua silaha za nyuklia